Meli
ya Kisasa Kuzinduliwa Karibuni na Kampuni ya Azam MarineMeli ya kisasa
karibuni kuzinduliwa inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo
tani 500.
KAMPUNI ya Usafiri wa baharini
ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwa ajili ya
abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo
Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu
wa mita 100 itazinduliwa. Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua
kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria
1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda
na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.
Waziri Mwenye dhamana ya
Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi
Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo
alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na
siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20
Chanzo: Zanzinews
Comments