Rais Barack Obama na mkewe Michele wameelezea masikitiko yao kufuatia mauawaji ya watu kumi na wanne mjini denver huko colorado.
Obama
alisema kuwa serikali itafanya kila juhudi kuwasaidia watu wa eneo la
tukio, la Aurora wakati huu mgumu.Alikiri kuwa serikali itakahakikisha
aliyehusika anakamatwa.
Mtu
mmoja aliyekuwa amefunika uso wake kwa barakoa aliwauwa kwa kuwapiga
risasi watu hao kumi na wanne na kuwajeruhi takriban hamsini wakati wa
onyesho la filamu ya Batman,The Dark Knight Rises.
Walioshuhudia
tukio hilo kwenye kitongoji cha mji huo cha Aurora walisema mtu huyo
aliyekuwa amevalia kifaa cha kujikinga dhidi ya gesi aliingia ndani ya
ukumbi huo na kurusha gesi ya kutoa machozi. Pindi gesi ilivyojaa
kwenyen ukumbi huo mshukiwa akaanza kuwafyatulia waliokuwemo risasi.
Comments