KATIBU MKUU AZILIPUA KAMPUNI ZA MAFUTA, ASEMA HAKUNA MGAWO WA UMEME
Waziri wa Nishati na Madini, Pofesa Sospeter Muhongo |
Mwandishi Wetu
WAKATI baadhi ya wabunge
wakitaka kuwachukulia hatua Waziri wa Nishati na Madini, Pofesa
Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakimu Maswi kwa madai ya
kuiuka sheria ya Ununuzi wa Umma, mtendaji mkuu huyo wa wizara ametupa
kombora la ufisadi dhidi ya baadhi ya kampuni za mafuta nchini.
Wanaowatuhumu akina Muhongo na Maswi wanadai kuwa, walikiuka sheria ya ununuzi wa umma kwa kuipa zabuni Kampuni ya Puma Energy ya kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL na kuziweka kando kampuni zilizokuwa zimechaguliwa kupitia mchakato halali wa zabuni ya Tanesco.
Wanaowatuhumu akina Muhongo na Maswi wanadai kuwa, walikiuka sheria ya ununuzi wa umma kwa kuipa zabuni Kampuni ya Puma Energy ya kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL na kuziweka kando kampuni zilizokuwa zimechaguliwa kupitia mchakato halali wa zabuni ya Tanesco.
Suala hilo linahusishwa na
kusimamishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, William Mhando kwamba
alichukuliwa hatua baada ya kukataa kutii maelekezo ya Wizara.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti
hili unaonyesha kuwa kumekuwa na mgawanyiko miongoni mwa wabunge, ambao
unaanzia kwenye Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo hadi sasa
hawajaafiki uamuzi wa kuwachukulia hatua viongozi hao.
“Ni kama tumeshindwa kuelewana
huko kwenye Kamati, lakini wabunge ndio tumekuwa tukilalamikia ufisadi
Tanesco, sasa tunawashangaa wenzetu ambao wameanza kuiandama tena
Serikali kwa kuchukua hatua,” alisema mmoja wa wabunge wa CCM.
Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa CCM alisema kuwa, Muhongo na Maswi walikiuka sheria.
“Tutakuwa tunakosea, tukiruhusu hawa watu wavunje sheria na halafu eti tuwaachie,” alsema mbunge huyo.
Nje ya Kamati hiyo, wabunge
bila kujali itikadi zao nao wamegawanyika huku wengine wakitaka
viongozi hao wachukuliwe hatua kuhusiana na suala hilo na wengine
walisema: “Hakuna kosa walilofanya, waachwe waendelee na kazi.”
Chanzo cha mgawanyiko huo ni
sababu zilizotolewa na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kwamba
waliwapa Tanesco fedha za kununua mafuta mazito ili kuiepusha nchi na
mgawo wa umeme, lakini wakaelekeza mafuta hayo yanunuliwe Kampuni ya
Purma ambako bei ya lita moja ni Sh1,460.
Comments