BAADA YA ABOUTRIKA NA MISRI: SASA NI VITA YA DROGBA NA DEMBA BA - SENEGAL VS IVORY COAST NANI KUIKOSA AFCON 2013?
Kutolewa kwa Mafarao hivi karibuni kwenye kuelekea AFCON 2013 kumestua wengi, huku kukiwa hakuna shabiki yoyote ambaye aliyekuwa akitegemea kwa mabingwa hao wa mara saba kutolewa na Afrika ya Kati ambao hawajawahi hata kushiriki kwenye michuano hiyo.
Egypt pembeni, kuna timu nyingine kubwa ambazo mashabiki wengi watapenda kuona wakishiriki kwenye michuano hiyo itakayofanyika Afrika Kusini mwakani January, lakini kwa hakika baadhi ya vigogo watashindwa kwenda Bondeni 2013.
Mpambano kati ya wacheza fainali wa 2012 Ivory Coast na magwiji wenzao wa soka wa Afrika Magharibi watapambana wenyewe kwa wenyewe na mmoja wao itabidi abaki kuangalia michuano hiyo kwenye TV, pia wapinzani wa kaskazini Algeria na Libya mmoja ataenda South Africa huku mwingine akibaki nyumbani.
Cameroon na Nigeria ambao wote walishindwa kuingia kwenye michuano ya 2012 ya AFCON, wanaonekana wameepuka balaa raundi hii kufuatia kuwa wapinzani ambao sio wagumu sana - zikicheza na Liberia na Cape Verde.
Wakati Zambia na Ghana wamepewa kukipiga na Uganda na Malawi, Gabon wataumana na Togo, huku Sierra Lione wakipigana vita na Tunisia.
Mpaka sasa hakuna timu yoyote yenye uhakika wa asilimia 100 kwenda South Africa, tunaweza kuapata mishangao mingi zaidi tukiwa tunaelekea kwenye hatua ya mechi za kufuzu kwani lolote linaweza kutokea, lakini ikiwa Senegal watacheza AFCON 2012 basi ni dhahiri Tembo wa Afrika watabaki Abdijan kuangalia michuano hii kwenye TV kama akina Kaseja.Inatoka /www.shaffihdauda.com
Comments