MWEZI MTUKUFU: Machangu wala Kichapo na Viboko Vya Nguvu huko Kinondoni Ni Kutoka Kwa Kikundi Cha Jumuia Ya Uamsho Tanzania Bara!
Machangu wamekiona cha mtemakuni! Wakati Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan ukiwa katika chungu cha nane, akina dada wanaofanya biashara
haramu ya kuuza miili maarufu kama Machangudoa au Chipsi Funga au Wauza
Sukari Tamu, wamekula viboko laivu baada ya kutuhumiwa kuwatega
Waislamu.
Tukio hilo lilijiri katikati ya wiki hii ambapo vijana wa Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania Bara walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia fimbo machangu ambao kwa sasa wametapakaa kila kona jijin
Tukio hilo lilijiri katikati ya wiki hii ambapo vijana wa Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania Bara walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia fimbo machangu ambao kwa sasa wametapakaa kila kona jijin
WATUMIA BAJAJ
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba.
BARABARA YA SHEKILANGO
Vijana
hao waliolenga kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo
walianzia kwenye Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viunga vya
Sinza, Dar ambapo kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi
kwenye mataa ya Shekilango waliwakuta machangu na kuwatandika viboko
kabla ya kutua mitaa ya Mwenge.
KINONDONI
Baada
ya kufagiafagia Sinza kwa kuwaadabisha wanawake hao ndipo zoezi
likahamia mitaa ya Kinondoni ambapo nao walipokea bakora za kutosha huku
wengine wakitoka nduki.
KISA KUHARIBIWA SWAUMU
Kwa
mujibu wa vijana hao, walifikia hatua ya kufanya zoezi hilo baada ya
muumini mmoja wa kiume kukatiza maeneo ya Corner Bar, Afrika Sana na
kuvutwa kisha kuchezewa nyeti na makahaba na kusabisha kuharibika kwa
swaumu yake.
Ilielezwa
kuwa baada ya kukutwa na kimbembe hicho, ilibidi muumini huyo kukatiza
safari yake ya kwenda kuswali msikikini mishale ya saa 2:00 usiku.
Ilisemekana
kuwa aliporudi nyumbani alitawadha na kufunga safari nyingine ya
msikitini na alipofika kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo akawasimulia
waumini wenzake ambao nao walikasirishwa na kitendo hicho hivyo
wakapanga kuvamia maeneo yote ya biashara hiyo ili kuwashikisha adabu.
Waandishi
wetu, wakiwa kwenye mishemishe zao za kutafuta habari mishale ya saa 5
usiku waliwashuhudia waumini hao wapatao saba wakishuka kwenye Bajaj
nyeusi maeneo ya Sinza wakiwa na bakora mikononi kisha kuwavaa machangu
hao na kuwatandika.
Wakati wakitekeleza zoezi hilo, jamaa hao walisikia wakiwaambia: “Sisi tupo kwenye swaumu nyiye mnatutega, ala!”
HAWAHESHIMU MWEZI MTUKUFU?
Waumini
hao waliongeza kuwa makahaba hao wamekuwa hawaheshimu mwezi huu
Mtukufu wa Ramadhan ndiyo maana wanaendeleza biashara yao hiyo ya aibu.
www.globalpublishers.info
Comments