MCHEZA filamu nyota wa Marekani, Sylvester Stallone ‘Rambo’ juzi aliwaongoza ndugu na jamii katika mazishi ya mtoto wake, Sage.
Sage (36) alifariki dunia wiki iliyopita kwa kile kinachodaiwa kuwa ni utumiaji uliokithiri wa dawa za kulevya.
Ibada ya mazishi ya Sage ilifanyika katika kanisa la St Martin lililopo Brentwood na mazishi yake yalifanyika katika makaburi ya Westwoodmjini Los Angeles.
Muda wote wa ibada na mazishi ya mtoto huyo, Rambo alionekana akitokwa na machozi.
Rambo (66) alikuwa amevaa suti nyeusi, tai nyeusi na shati jeupe. Pia alikuwa amevalia miwani myeusi.
Katika mazishi hayo, Rambo alikuwa ameongozana na mke wake wa sasa, Jennifer Flavin.
Mke wa zamani wa Rambo na mama wa Sage, Sasha Czack naye alikuwepo kwenye mazishi hayo pamoja na mtoto mwingine wa mcheza filamu huyo, Frank.
Mashabiki mbali mbali wa Rambo pia walishiriki katika mazishi hayo wakiwa wamebeba maua na picha zake pamoja na za Sage.
Sage alikuwa akiwa amekufa nyumbani kwake wiki iliyopita, pembeni yake kuwa na chupa kadhaa za vidonge.
Rambo ameelezea kusikitishwa kwake kutokana na msiba wa Sage, ambao alikiri kwamba ni pigo kubwa kwa familia yake.
Comments