BARAZA
la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa),
limerudisha nyuma siku moja mechi michuano ya Kombe la Kagame kati ya
Simba dhidi ya URA kutoka Jumatatu hadi Jumapili.
Akizungumza
na wanahabari Katibu mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye alisema mchezo
kati ya Simba na URA ya Uganda sasa utafanyika Jumapili.
Awali
mchezo huo ulipangwa kufanyika Jumatatu kutokana na uwanja wa Taifa
kutumika kwa fainali ya michuano ya Copa Coca Cola, lakini sasa mechi
hizo sasa zimehamishiwa uwanja wa Karume.
Musonye
alisema mbali na mechi za Simba na URA pia mechi nyingine itakayochezwa
Jumapili ni ile ya Vita Club ya DR Congo dhidi ya Ports ya Djibout
ambayo itafanyika saa nane mchana kwenye uwanja wa Azam Chamazi.
"Katika
uwanja wa Chamazi kutakuwa na mechi nyingine itakayoanza saa 10 kamili
jioni, itakayowakutanisha wenyeji Azam ya Tanzania Bara dhidi Mafunzo
kutoka Zanzibar."
Chanzo:www.mwananchi.co.tz
Comments