Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (katikati) akisisitiza jambo katika hafla hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (kulia), akimkabidhi hundi
ya shilingi milioni 10, Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Mamlaka ya Elimu
nchini (TEA), Seif Mohammed.
Seif Mohammed (kushoto), akiishukuru Global Publishers na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kuchangia mfuko huo.
Kampuni
ya Global Publishers & General Enterprises Ltd leo imetoa hundi ya
shilingi milioni 10 ikiwa ni sehemu ya mapato yaliyopatikana kwenye
Tamasha la Matumaini lililoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya
kuchangia ujenzi wa hosteli za wasichana nchini. Kampuni hiyo imetoa
hundi hiyo kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Atriums
iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)
Comments