Watanzania
ni wakati sasa wa kujivunia mafanikio ya baadhi ya watanzania
wanaofanya vizuri katika viwango vya kidunia, katika historia ya michezo
tangu tupate uhuru ni Hasheem Thabeet pekee ndio ameweza kufanikiwa na
kucheza ligi ya juu kabisa duniani katika michezo.
Wako
watanzania wengi wamefanikiwa katika michezo mbali mbali na kufanikiwa
kucheza katika ligi za michezo mbali mbali na katika nchi mbali mbali
ila kila mchezo una ligi zake ambazo ni za kiwango cha juu juu kabisa ni
yeye pekee ndio amweza kufanya hivyo kwa kufanikiwa kucheza mfululizo.
Hasheem
amecheza timu za Memphis na baadae kucheza Houston Rockets na mwishoni
mwa msimu uliopita alicheza Portland Trail Blazers. Katika timu ya
Blazers alicheza michezo yote 16 liyokuwa imebaki kabla ya msimu
kumalizika.
Hasheem kwa sasa ndio mwafrika mwenye kiwango cha juu kabisa miongoni mwa waafrika wanaocheza kikapu Marekani na ni mchezaji pekee anayecheza huko toka ukanda wa Afrika , Mashariki, Kati na Kusini.

Hasheem ni mchezaji wa Afrika ambaye ameingia NBA akiwa
na kiwango cha juu kabisa katika historia ya mchezo huo, yaani No. 2 NBA
Draft ya 2009.
Kwa Hasheem kuchukuliwa na timu kama Oklahoma City ambao ni mabingwa wa kanda ya magharibi ya NBA na mwaka huu walicheza fainali ya ubingwa wa NBA na kushindwa na Miami Heat, inaonyesha jinsi ambavyo bado mchezaji huyo anathaminiwa na bado uwezo mkubwa wa kuisaidia timu kubwa kama OKC ili iweze kufikia malengo yake.
Hivyo basi kwetu sisi Tanzania tunampongeza na kujivunia mafanikio hayo. Hasheem pia amekuwa ni mchezaji pekee wa kiwango cha juu ambaye amekuwa akirudisha fadhila nyumbani na kila anapopata mapumziko huwa anarudi nyumbani kuja kushirikiana na watanzania wenzake ili kuwainua na kuibua vipaji.
Kwa niaba ya shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania, natoa pongezi nyingi kwa Hasheem na tunamtakia kila heri na tumuombee kwa Mungu ili afanikiwe zaidi katika kikapu.
Mungu Mbariki Hasheem, Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Phares Magesa

Makamu wa Rais
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF)
Comments