
Taarifa nzuri ni kwamba mabingwa hao wa Spain watakuwa wakifanya mazoezi kwenye sehemu ya wazi kwa wale ambao wangependelea kuwaona: habari mbaya ni kwamba itabidi uichimbue sana mifuko yako kuweza kulipia kuwaona Ronaldo na wenzie wakifanya mazoezi. Gharama za tiketi kuwaona Madrid zimepanda mpaka kufikia €311 kwa kipindi cha saa moja na nusu kuweza kumshuhudia Mourinho akitoa maelekezo huko Los Angeles mwezi August tarehe 4.
Tiketi ya bei rahisi itagharimu kiasi cha €69, lakini tiketi ya gharama zaidi itakayokuwa ikihusisha kupata breakfast pamoja na kuweza kukutana na wachezaji na kuongea nao itarudi na kufikia €311 ambayo ni sawa na kiasi kisichopungua 650,000 za kibongo.
Na kama utapenda kuangalia mazoezi na kwenda kuangalia mechi ya kirafiki dhidi ya LA Galaxy, then itabidi uongeze €448 .inatoka www.shaffihdauda.com
Comments