Skip to main content

AY kupiga collabo na staa wa The X Factor USA




MTANDAO mmoja wa jamii unaeleza kuwa mwana  commercial hataki mchezo kabisa sasa hivi. Lengo lake ni kuvuka border tu. Mazungumzo ya wazi kwenye mtandao wa Twitter kati ya Ambwene Yesaya na meneja wake Hemdee Kiwanuka yanaashiria kuwepo kwa collabo nyingine ya kimataifa ya AY hivi karibuni.
Kwa mujibu wa mazungumzo hayo, mshiriki wa shindano maarufu la The X Factor USA  Chris Rene yupo tayari kupiga collabo na Ay.
“Check Out Chris Renee... We got him for a collabo anytime. That's why I wanted you at Sean's Concert, for networking,” ametweet Hemdee.


Chris Rene
Kama alivyomalizia hapo mwisho, Hemdee anamtaka AY awepo kwenye concert ya Sean Kingston ambayo hata hivyo haijulikani itafanyika wapi na lini, ili kuongeza network na wasanii wakubwa.


Hemdee
Christopher "Chris" Rene aliyezaliwa mwaka 1982 alishiriki kwenye msimu wa kwanza wa shindano la The X Factor USA na alikuwa mshindi wa tatu nyuma ya Melanie Amaro na Josh Krajcik.

Comments