Wananchi
wa Norway wamekusanyika katika makao makuu ya serikali mjini Oslo
Jumapili (22.07.2012) kwa ajili ya kumbukumbu ya watu 77 waliouliwa na
Anders Breivik katika shambulio la bomu na risasi mwaka mmoja uliopita.
Waziri Mkuu Jens Stoltenberg
ameuambia umati uliokusanyika kwenye kumbukumbu hiyo kwamba "Bombu na
risasi hizo zilikuwa zimekusudia kuibadili Norway.Wananchi walijibu kwa
kufumbata maadili yetu.Muuaji huyo ameshindwa na wananchi ndio
walioshinda".
Breivik ambaye alisema wahanga
wake ambao takriban wote walikuwa vijana wadogo walikuwa wasaliti kwa
sababu waliunga mkono mchanganyiko wa utamaduni na uhamiaji wa
Waislamu,aliripua bomu nje ya bunge na kuuwa watu wanane.
Kisha akawauwa kwa kuwapiga risasi watu wengine 69 katika kambi ya vijana ya chama tawala cha Labour katika kisiwa cha Utoeya.
Ni vigumu kusahao
Vegard Groeslie Wennesland
muhanga wa mauaji ya Utoeya amesema "Ni watu wachache wanaweza kupitisha
siku bila ya kufikiria yale yaliotokea tarahe 22 mwezi wa Julai"
Anasema aidha utakuwa unamjuwa
mtu fulani ambaye sasa hayuko tena,rafiki, mshauri au kitu fulani
ambacho kinakukumbusha yale yaliotokea.
Comments