Bondia Francis Cheka jana aligoma kupanda ulingoni kuzipiga na Japhet
Kaseba kwa madai kuwa, mpinzani wake hana sifa za kucheza naye.
Cheka alitoa madai hayo baada ya kuzungukwa na waandishi wa habari waliotaka kujua kwa nini amegoma kupigana na Kaseba wakati alishalipwa fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
Kaseba alishapanda ulingoni tayari kwa ajili ya pambano hilo, lakini Cheka aliingia ulingoni akiwa amevaa nguo za kawaida na kuomba kipaza sauti ili azungumze, lakini alinyimwa.
Kuona hivyo, Cheka aliamua kushuka ulingoni huku waandaaji wa pambano hilo pamoja na mashabiki wakionekana kumshangaa kutokana na uamuzi wake huo.
Cheka alidai kuwa, mpinzani wake hana sifa za kupigana naye kwa sababu amepigana mapambano matatu, kapigwa mawili hivyo sio saidi yake.
Aliitaja sababu nyingine kuwa ni mpinzani wake kuwa na uzito mdogo, hivyo kisheria isingekuwa sahihi kupigana naye.
Hata hivyo, Cheka alishindwa kuwaridhisha mashabiki baada ya kukataa kujibu swali lililomtaka aeleze kwa nini alitia saini mkataba wa kucheza pambano hilo na kuchukua fedha za waandaaji.
Bondia Francis Cheka akitoka ulingoni baada ya kugoma kuzipiga na Japhet Kaseba wakati wa tamasha la matumaini lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Comments