Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi-Zanzibar
Jeshi la Polisi Zanzibar
linawashikilia wafanyakazi sita wa meli ya MV Skagit akiwemo mmiliki
wake Bw. Said Abdulrahman pamoja na Nahodha wa meli hiyo Bw. Mussa
Makame Mussa na wanahojiwa kufuatia tukio la ajali ya meli hiyo
iliyosababisha vifo vya baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kutoka
Bandari ya Dar es Salaam kwenda Bandari ya Zanzibar.
Watuhumiwa
hao walikuwa wakihojiwa katika Ofisi za Upelelezi Makao Makuu ya Jeshi
la Polisi mjini Zanzibar ambapo Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai
Zanzibar, ACP Yusuph Ilembo, amesema watuhumiwa hao wawataweza
kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Kamanda Ilembo amesema kuwa
Makachero wa Jeshi la Polisi wanaendelea na uchunguzi na kutafuta
taarifa nyingine zinazohusiana na tukio hilo.
Hata hivyo, Nahodha wa zamu siku
ya tukio hilo la kupinduka na kuzama kwa meli hiyo ya MV Skagit,
Bw.Mussa Makame Mussa, ameelezea kwa ufupi jinsi ajali hiyo ilivyotokea
na namna yeye alivyonusurika katika ajali hiyo.
Amesema kuwa ajali hiyo ilitokea
baada ya kupigwa na dharuba na mawimbi yaliyoambatana na upepo mkali,
ambapo yeye alinusurika kufa maji baada ya kuruka kwa kutumia mlango wa
mbele wa meli hiyo na kuanza kuogelea ambapo alijichanganya pamoja na na
abiria wengine walionusurika na kuokolewa na vyombo vya uokozi.
Wakati huo huo, Wapiga mbizi wa
Vikosi vya Ulinzi na usalama leo wamefanikiwa kuzupata maiti ngingine za
watu watano akiwemo mwanamke mmoja na wanaume wanne.
Katika upekuzi wa maiti hizo,
Makachero wa Polisi walibaini kitambulicho cha kupigia kura kutoka kwa
mmoja ya mwili wa marehemu kitambulicho kilichokuwa na jina la Philip
John Busiya aliyezaliwaq mwaka 1977 katika kijiji cha Mapilinga
kilichopo katika Kata ya Igokelo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Comments