Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema Somalia ni lazima
imalize kipindi cha mpito katika tarehe iliyopangwa, huku likionyesha
wasiwasi mkubwa kutokana na muda huo kuzidi kuelekea ukingoni.
Baraza hilo limeitaka serikali ya mpito pamoja na viongozi wa siasa nchini Somalia kuongeza juhudi na kutimiza matakwa yote yanayotakiwa kufikia tarehe 20 mwezi ujao (Agasti) ambao ndio muda wa mwisho uliopangwa.
Somalia imekuwa na serikali ya mpito tangu mwaka 2004 lakini haijapata serikali kamili tangu mwaka 1991. Baraza la usalama lilitangaza tarehe hiyo mwezi Februari na kutoa wito kwa pande zote kutimiza makubaliano hayo yenye lengo la kuimarisha hali ya usalama, kuunda serikali kuu, pamoja na kuandika katiba.
Baraza hilo limeukaribisha mkutano wa bunge uliofanyika jana. Bunge la Katiba la Somalia lilikutana mjini Mogadishu hapo jana baada ya kuwa limeahirishwa mara kadhaa huko nyuma.
Kikao cha kwanza cha Bunge
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Abdullahi Osman, amesema kuwa wajumbe wote 825 walioteuliwa kupitisha katiba walihudhuria. Wengine waliohudhuria kikao cha jana ni Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali na Spika Sheikh Sharif Hassan Aadan.

Comments