MFUMKO wa bei umeshuka kutoka asilimia 18.2 hadi 17.4, kati ya Mei na Juni mwaka huu.
Taarifa kwa umma iliyotolewa
Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu, Dk Albina Chuwa
anasema kupungua kwa mfumko wa bei Juni mwaka huu, inaonyesha kasi ya
upandaji bidhaa imepungua.
Dk Chuwa alisema mfumko wa bei wa vyakula na vinywaji baridi umepungua hadi kufikia asilimia 23.5 kutoka asilimia 25.3.
“Mfumko wa bei ambao
haujumuishi vyakula na nishati kwa Juni mwaka huu, umeongezeka hadi
asilimia 8.8 kutoka asilimia 8.7 Mei mwaka huu,” alisema Dk Chuwa.
Kwa upande mwingine, mfumko wa bei ya nishati umepungua hadi asilimia 20.5 kutoka asilimia 21.2.
Alisema
mfumko wa bei umekuwa na mwenendo wa kupanda kutoka asilimia 10.9 hadi
asilimia 19.8, kati ya Juni na Desemba, mwaka jana.
“Kuanzia Januari mwaka huu mwenendo wa mfumko wa bei ulianza kushuka kutoka asilimia 19.7 hadi asilimia 17.4,” alisema Dk Chuwa.
Maboresho yamefanyika kwenye ukokotoaji bei za taifa, kuanzia ngazi za mwanzo.
Thamani ya Sh100 imepungua kutoka Septemba mwaka jana hadi Sh76.89, Juni mwaka huu.
Comments