POLISI KUWAHOJI KWA MATAMSHI KWAMBA WANATISHIWA MAISHA, DK NCHIMBI ASEMA WANASABABISHA CHUKI
Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Willibrod Slaa |
Neville Meena na Florence Majani, Dodoma
KATIBU
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na
Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema huenda wakajikuta
matatani kutokana na madai waliyoyatoa juzi kwamba wanatishiwa kuuawa
na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Kutokana na matamshi hayo, jana Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ameliagiza Jeshi la Polisi kuwahoji viongozi hao ambao walidai kuwa mauaji hayo yamepangwa kufanywa kwa kuwekewa sumu kwenye chakula au kwa kutumiwa makundi ya ujambazi.
Kutokana na matamshi hayo, jana Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ameliagiza Jeshi la Polisi kuwahoji viongozi hao ambao walidai kuwa mauaji hayo yamepangwa kufanywa kwa kuwekewa sumu kwenye chakula au kwa kutumiwa makundi ya ujambazi.
Akizungumza na waandishi wa
mjini hapa jana, Dk Nchimbi alisema licha ya kudai kwamba wanatishiwa,
ameshangazwa na msimamo wa viongozi hao kukataa kupeleka suala hilo
polisi kwa madai ya kuhofia suala hilo halitafanyiwa kazi.
Alisema watawahoji viongozi hao
kwa sababu suala la usalama wa Mtanzania yeyote si la hiari, bali ni la
kikatiba na la kisheria hivyo, ni lazima polisi watimize wajibu wao.
“Ni lazima tuwahoji ili tujue
ni nani amewatisha na kwa sababu zipi. Hatutamuomba mtu ruhusa ya
kumlinda kwa sababu huo ni wajibu na kazi yetu kuwalinda raia, hilo
halina mjadala. Hatua zitachukuliwa endapo itabainika kuwa madai yao
yana ukweli,” alisema Dk Nchimbi.
Aliwataka viongozi wote wa
kisiasa wakiwamo wa Chadema wanapohisi kutishiwa usalama wao, watoe
taarifa polisi ili vyombo vya dola viyafanyie uchunguzi malalamiko yao
ili utaratibu ufanyike kuhusu usalama wao kama sheria inavyotaka.
Alionya tabia ya viongozi
kuzungumza nje ya utaratibu akisema haikubaliki kwani inaweza kuwa ni
mbinu za kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
Comments