Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa DK Asha-Rose Migiro |
Raymond Kaminyoge
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk Asha-Rose Migiro ambaye anarejea nchini leo ametoa waraka maalumu akisema mwisho wa utumishi wake katika umoja huo ni mwanzo utekelezaji wa majukumu mengine hapa nchini.
Kauli ya Dk Migiro imekuja kipindi ambacho jina lake limekuwa likitajwa katika nafasi ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete atakapomaliza muda wake wa kuongoza taifa mwaka 2015. Kabla ya kwenda UN, Dk Migiro alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Dk Migiro ambaye aliteuliwa na Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-Moon kushika mwaka 2007 wadhifa huo, alisema anafurahi kumaliza miaka mitano kwa mafanikio.
Katika waraka huo ambao gazeti hili limeuona jana, Dk Migiro alisema: “Hakika, kila chenye mwanzo hakikosi mwisho na kila mwisho wa jambo moja huwa mwanzo wa jingine.”
Alisema ingawa ni mapema kwake kutoa tathmini halisi ya utendaji wake kazi, wadhifa huo katika Umoja wa Mataifa umempatia uzoefu mkubwa.
“Kukitumikia chombo hiki cha kimataifa kwa muda wa miaka mitano na nusu mfululizo ni heshima ya pekee ambayo daima nitaienzi kama kilele kimojawapo cha mafanikio katika maisha yangu ya utumishi wa umma. Kila siku niliyoitumia katika Umoja huo ilikuwa ni darasa la kusukuma mbele mipaka ya ujuzi na elimu,” alisema Dk Migiro.
Alisema amefahamu mambo mengi kuhusu umoja huo, dunia na watu wake ikiwamo ukomo wa umoja huo katika kushughulikia matatizo mbalimbali yanayoikabili dunia.

Comments