Mshambuliaji John Bocco ndiye
aliyeibuka shujaa wa Azam baada ya kuifungia mabao yote matatu, moja
kipindi cha kwanza na mengine kipindi cha pili. Bao pekee la Simba
lilifungwa na Shomari Kapombe.
Ushindi huo umeiwezesha
Azam kutinga nusu fainali, ambapo sasa itakutana na AS Vita ya Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo. Vita imefuzu kucheza hatua hiyo baada ya
kuitoa Atletico ya Burundi mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa kuanzia
saa nane mchana.
Mechi nyingine ya nusu fainali
itazikutanisha Yanga na APR ya Rwanda. Yanga imetinga hatua hiyo baada
ya kuitoa Mafunzo ya Zanzibar kwa penati 5-3 wakati APR iliitoa URA ya
Uganda kwa mabao 2-1.
Kwa mujibu wa ratiba, mechi zote
mbili za nusu fainali zitachezwa Alhamisi wiki hii. Mechi ya kwanza
itazikutanisha Azam na APR wakati katika mechi ya pili, Yanga itavaana
na AS Vita.
Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kupigwa Jumapili, ikitanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.Inatoka kwa mdau.
Comments