Manji, Sanga, Katabalo na Bin Kleb wakijadiliana jambo kabla ya kuzungumza na wachezaji
Mwenyekiti
wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji jana ametembelea tena makao makuu ya
klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kuzungumza na
wachezaji.
Viongozi hao walikutana na
wachezaji kwa saa kadhaa na kuzungumza nao mambo mbalimbali kwa lengo la
kuwaweka sawa kabla ya mechi yao ya robo fainali ya michuano ya Kombe
la Kagame dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.
Yanga inatarajiwa
kushuka dimbani leo kucheza na Mafunzo katika mechi ya pili ya robo
fainali itakayoanza saa 10 jioni. Katika mechi ya awali, URA ya Uganda
itavaana na APR ya Rwanda.Inatoka kwa mdau.
Comments