Umati wa Wapenzi wa muziki wa Injili walioingia katika uzinduzi wa albamu ya Hakuna jipya ya msanii mchekeshaji Masanja Mkandamizaji katika Uwanja wa Samora Iringa.
Masanja Lucas Mgaya amesema kuwa wamefurahi sana kwani mwito ulikuwa
mkubwa japo onyosho lenyewe lilikuwa limeandaliwa kwa muda mfupi lakini
watu walijitokeza kwa wingi na kuhudhuria tamasha hilo lilokusanya
wakazi kutoka Ipogolo, Kihesa, Kwa semtema, Mkwawa, Ruaha, Kibwabwa,
Igangilonga, Wilolesi, Kitanzani na Ilala.“Kazi nzuri naweza sema
tumefanikiwa kwa kuweza kuwaleta wapenzi wa muziki wa Injili na
kusherekea vizuri, onyesho lilienda vizuri, tumeanza na uzinduzi wa
Albamu ya Hakuna Jipya nyumbani kisha tunaelekea Dodoma kwa ajili ya
kuhubiri neno la Mungu kwa njia ya muziki wa Injili,”anasema
Lucas.Uzinduzi wa albamu ya Hakuna Jipya ulisindikizwa na waimbaji
wakali kama Martha Mwaipaja, Masanja akisindikizwa na rafiki yake wa
karibu Silas Mbise, katika uwanja wa Samora ulipamba na nyota wa filamu
Nchini kutoka Bongo movie club walipagawisha wapenzi wa filamu za
kibongo.
Comments