..Mashabiki wakisubiri Dogo Janja awasili kutoka Arusha.
Dogo Janja akiwa kabebwa na mashabiki wake pamoja na baadhi ya wasanii wa kundi la Mtanashati.
Janja akiwa na PNC baada ya kuwasili jijini Dar.
PNC akibebwa baada ya kupoteza fahamu wakati wa shamra shamra za kumkaribisha Dogo Janja.
Mashabiki wa Dogo Janja wakiwa na mabango ya kumkaribisha.
Dogo Janja akiwa kwenye gari kuelekea makao makuu ya kundi la Mtanashati Entertainment.
Msanii chipukizi wa muziki wa Hip Hop, Abdulaziz Chende maarufu kwa
jina la Dogo Janja, leo amerudi jijini Dar es Salaam na kujiunga na
kundi la Mtanashati Entertainment. Mwanzo Dogo Janja alikuwa kundi la
Tip Top Connection linaloongozwa na Madee lakini ilitokea kutoelewana
kati yao na kurudishwa kwao Arusha. Janja karudi jijini kwa ndege ya Air
Tanzania na anataraji kusaini mkataba na kundi hilo la Mtanashati
kuanzia sasa.(PICHA ZOTE NA ERICK EVARIST WA GPL)
Comments