Bingwa
mara tano katika mashindano ya tennis ya Wimbledon, Mmarekani Venus
Williams, amesema hana nia ya kustaafu, baada ya kuondolewa katika siku
ya kwanza ya mashindano ya mwaka 2012 ya Wimbledon, katika raundi ya
kwanza, aliposhindwa na mchezaji kutoka Urusi, Elena Vesnina.
Venus, mwenye umri wa miaka 32, na anayeugua ugonjwa unaofahamika kama Sjogren's Syndrome, alishindwa 6-1 6-3 siku ya Jumatatu.
Mpinzani wake Vesnina amepangwa katika nafasi ya 79 katika orodha ya wachezaji bora zaidi wa tennis wa kike ulimwenguni.
"Haiwezekani nipumzike tu na kukata tamaa," alielezea Williams.
"Sina muda wa kujisikitikia. Hilo sio jambo zuri. Nitautumia muda wangu katika mawazo yanayonipa nguvu. Ninaupenda mchezo huu."
Mara
ya kwanza Williams kushindwa katika raundi ya kwanza ilitokea mwaka
1997, wakati alipoingia pambano lake la kwanza la Wimbledon, na wakati
huo alikuwa hata hayumo miongoni mwa wale waliopangwa katika mashindano
hayo kama wachezaji bora.
Ni wanawake
wawili tu ulimwenguni ambao wameshawahi kupata ubingwa wa Wimbledon
mara nyingi kumshinda Williams, lakini tangu mwaka 2008, hajawahi
kuibuka bingwa wa mashindano hayo.
Mara tu baada ya ushindi wake wa mwisho, iligunduliwa kwamba anaugua ugonjwa wa Sjogren's Syndrome, na ambao humfanya mgonjwa kujihisi ni mchovu mno, na katika sehemu mifupa inaungana, maumivu.Source BBC.
Comments