Mwili wa aliyekuwa Katibu msaidizi wa Chama cha Mpira wa miguu
wilaya ya Nyamagana (NDFA) marehemu Osward Mchopa umeagwa leo katika
viwanja vya Nyamagana na mamia ya wananchi pamoja na wanamichezo
ikiwemo viongozi wa serikali na wadau wa michezo jijini Mwanza.
Mbele kabisa ameketi diwani wa kata ya Nyamagana Bihku Kotecha kweye jukwaa kuu na wahudhuriaji heshima za mwisho kwa mdau huyo wa soka mkoani Mwanza.
Sehemu ya Umma:- Marehemu Mchopa alizaliwa mwaka 1958 wilayani Newala mkoani Mtwara, akiwa mtoto wa nne katika familia ya Mzee Simon Mchopa ambaye alianza maisha ya soka wilayani Tunduru aliichezea timu ya Kampuni iliyotwaa ubingwa.
Wadau wa michezo toka kona na kona wakifuatilia yanayojiri viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza leo:- Kwa mujibu wa historia mnamo mwaka 1982 marehemu aliajiliwa kama afisa Utamaduni daraja la tatu na Halmashauri ya Manispaa ya Mwanza ambayo sasa ni jiji na Mwaka 1994 alipunguzwa kazi na kujikita kufundisha Vijana walio na Umri chini ya miaka 14katika uwanja mkongwe wa Nyamagana hadi mauti yakimkuta alikuwa akifundisha timu mbalimbali jijini hapa.
Afisa Idara ya elimu jijini Mwanza akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Wadau mbalimbali toka sehemu na sehemu wamefulika viwanjani hapa kuuaga mwili wa marehemu:- Wakati wa uhai wake marehemu aliwahi kuzichezea timu za Manispaa ya Mwanza, Lumumba Rovers na ni mmoja kati ya makocha waliohudhuria mafunzo ya ukocha hatimaye kupewa dhamana ya kufundisha timu za Copa Coca cola, Mwanza Heros na timu ya vijana wadogo ya Toto Afrika jijini Mwanza.
Mwenye shati jeusi ni Khalfani Ngassa (baba yake na Mrisho Ngassa) mbele yake akiwa ameambatana na Venancy Kazungu wote wakiwa ni wachezaji wa zamani wa Pamba na timu ya mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye mstari kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mchopa.
Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoani Mwanza (mwenye t-shirt nyeupe) akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Kamati ya mazishi kutoka kulia ni mweka hazina wa Chama cha
soka mkoani Mwanza (MZFA)Ezrael Mtambalike, Katibu wa MZFA Mabrouk,
mdau wa Soka Mr. george, Katibu mkuu wilaya ya Nyamagana Munga Mpindo
na mkufunzi wa soka Nyamagana.
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa malaria na kifua
hali iliyopelekea kuzidiwa na kupelekwa hospitali ya Sekoutoure kabla
ya hali kuwa mbaya mnamo saa 6:00 usiku wa tarehe 16 juni 2012
alipoaga dunia. Marehemu amezikwa leo alasili katika makaburi ya
Nyashana jijini Mwanza.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.Inatoka kwa mdau.
Comments