Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika
akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania mapema leo mjini Dodoma baada ya
kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati
akichangia
Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano
unaoendelea.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma
......................................................................................
Nitatoa
tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa
bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini
Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino
mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la
mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye
baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita
ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia
kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri
mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu
ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina
mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana
mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa
Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe
marekebisho!
19 Juni 2012
Source: Jestina George Blog
Source: Jestina George Blog
Comments