Chama
Cha Mapinduzi (CCM) leo kimeiteka Songea baada ya umati wa wananchi wa
mji huo kujitokeza katika mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma. Pichani,
Nape akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye uwanja huo. Kushoto
ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Cornel Msuha. (Picha na Bashir
Nkoromo).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

Comments