KLABU ya Simba imefanikiwa kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Masombo Lino kutoka Daring Club
Motema Pembe.
Beki hilo la kati ambalo lilipiga soka ya
uhakika mwaka jana wakati Simba ilipokutana na DC Motema Pembe katika
mechi ya mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho
Afrika, lilitua jana Dar es Salaam na leo imeelezwa limesaini mkataba.
“Masombo
amekuja jana saa mbili usiku, alikuwa ana mzungumzo na Makamu
Mwenyekiti, inawezekana leo akawa amesaini mkataba wa miaka miwili kama
wameafikiana,”alisema Kamwaga.
Simba, mabingwa wa Ligi
Kuu ya Bara, wanamsajili beki huyo kuziba pengo la beki wao hodari,
Kelvin Patrick Yondan ambaye amehamia kwa wapinzani, Yanga.
Comments