Kongamano
linalojulikana kama Global Media Forum ambalo linawaleta pamoja
wataalamu kutoka vyombo vya habari, wanasayansi na wanasiasa, limeanza
leo Jumatatu (Juni 25 hadi 27 ) katika jengo la Deutsche Welle mjini
Bonn
" Elimu bado ni mada kuu katika
suala zima la utandawazi," alitamka hayo Mkurugenzi mkuu wa Deutsche
Welle, Erik Bettermann. Jinsi gani " Elimu kwa wote" lilivyo jambo
muhimu, ndiyo suala kuu la majadiliano ya siku tatu miongoni mwa
wataalamu kutoka vyombo vya habari, wanasayansi na wanasiasa kuanzia
Jumatatu (Juni 25 hadi 27 ) katika kongamano linalojulikana kama Global
Media Forum katika jengo la Deutsche Welle mjini Bonn." Habari na elimu
ndiyo msingi wa harakati za chombo cha matangazo ya kigeni cha
Ujerumani", anasema Mhariri mkuu wa DW, Ute Schaeffer.
Kwa mujibu wa idadi rasmi ya
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa mataifa, kiasi ya
watu 800 milioni hawajui kusoma na kuandika.Wakati huo huo, inaelekea
Ulimwengu ni jamii ya habari, ambayo kwa mujibu wa Erik
Bettermann,hutupa nafasi ya kupata maarifa kila wakati na popote tulipo.
Vyombo vya habari kutoa mwangaza
Ni kwa sababu hii hasa, vyombo
vya habari kote duniani vinawajibu. " Vina jukumu muhimu kama chombo cha
kutoa muwangaza ", anasisitiza Mkurugenzi mkuu wa DW. Kwa watu wa
tabaka mbali mbali katika Dunia ya utandawazi, elimu, utamaduni na elimu
kwa wote, yanaweza kuwa ni ufunguo wa kuweza kuishi pamoja kwa amani,
kwa maendeleo na majadiliano baina ya watu wa tamaduni mbali mbali.
Comments