Na Ashura Mohamed na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
BENKI ya CRDB imefanikiwa kuongeza utoaji wa mikopo yake kwa
asilimia 27, kufikia shilingi bilioni 1.4 kutoka shilingi bilioni
1.1 mwaka 2010.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB nchini, Dk.
Charles Kimei, wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kumi na saba wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika Jijini Arusha.
Aidha sekta ya kilimo imeongoza kwa kuchangia asilimia 30 ya mikopo
yote iliyotolewa na benki hiyo, huku ikifuatiwa na biashara na
viwanda kwa asilimia 14.
Pia alizitaja sekta zingine ambazo zimechangia ukuaji wa mikopo hiyo kuwa ni
Mikopo binafsi asilimia 12, Utalii, hoteli na migahawa asilimia 8, wakala wa masuala ya
kifedha asilimia 7,upangishaji majengo na ujenzi 6, mawasiliano na
uchukuzi kila moja asilimia 7. huduma za kijamii 6, uzalishaji na
usindikaji 3 na uchimbaji wa madini na kokoto asilimia 1.
Lakini hata hivyo alisema ukuaji huo umechangiwa na chapa ya Benki , ambayo imeendelea kuboreshwa kwa kampeni za masoko, kuanzishwa na kubuniwa kwa bidhaa na huduma mpya,kukua na kusambaa kwa njia za utoaji huduma.
Pia alisema pamoja na changamoto za uchumi zilizoikumba biashara na Benki,utendaji katika maeneo mengi umekuwa wa kuridhisha, kwa kuongeza ukopeshaji ambapo waliweza kuongeza pato lake la riba huku ikipunguza gharama za riba, kiasi cha kuzalisha pato halisi la riba la shilingi bilioni 157.4 ikilinganishwa na shilingi bilioni 125 kw amwaka uliopita.
Dk. Kimei alisema kuwa benki yao imejikita zaidi katika uwekezaji
katika jamii na udhamini kwa kutazama vipaumbele vya jamii, ambavyo ni
elimu, afya na mazingira huku nguvu kubwa ikielkezwa katika makundi
yaliyosahauliwa katika jamii na kuchangia wahanga wa majanga
yaliyoikumba nchi ndani ya mwaka 2010.
Alisema benki hiyo hadi kufikia sasa, wana mtandao wa matawi 82 ikiwa
pamoja na matawi yanayotembea, kwa angalau tawi moja, katika kila Mkoa
nchi nzima na wana mtandao (Internet) wa huduma za benki, ambazo
zinawafikia wateja 20,000 na huduma inayokua haraka kupitia simu ya
mkononi ikiwa na zaidi ya wateja 30,000, kufikia mwishoni mwa Desemba
2011
Comments