Waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania wakishiriki kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward. Mwili wa marehemu Willy unasafirishwa mchana huu kutoka Morogoro kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa kwa ushirikiano wa ndungu na viongozi wa Jambo Concepts, lakini kwa mujibu wa Kaka wa marehemu Rabach ni maaishi yatafanyika nyumbani kwao marehemu, mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara. Siku ya mazishi itatangazwa baadaye.
Mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema, akiwa kwenye majonzi
Akina mama waombolezaji wakiwa kwenye msiba
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto akihojiwa na Grace Kingarame wa TBC katika msiba huo. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA)
Comments