Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na viongozi wa mifuko
ya hifadhi ya Jamii na Shirika la Nyumba la taifa ikulu mjini Dodoma
leo.Katika kikao hicho Mheshimiwa Rais aliwapa changamoto viongozi hao
kuunganisha nguvu na kubuni mikakati itakayowezesha kuwapatia watumishi
wa umma nyumba za kuishi
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhani Dau akiteta Jambo na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu mjini Dodoma leo.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa NHC Bwana Nehemiah Mchechu mara baada ya kikao maalumu
kilichofanyika ikulu mjini Dodoma leo.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akiongea na
mkurugenzi mkuu wa PPF Bwana William Eriyo mjini Dodoma leo baada ya
kikao maalumu na viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la
Nyumba.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la Nyumba la Taifa mara baada ya
kikao maalumu kilichofanyika ikulu mjini Dodoma leo. viongozi Wengine
waandamizi w aliohudhuria kikao hicho Naibu Waziri wa Ardhi Goodluck
ole Medeye(watatu kushoto),Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni
Sefue(Wanne kushoto),Gavana wa Benki Kuu Professa Beno Ndulu(kulia) na
naibu katibu Mkuu Hazina Dr.Servacius Likwelile(kushoto). Katika kikao
hicho Mheshimiwa Rais aliwapa changamoto viongozi hao kuunganisha nguvu
na kubuni mikakati itakayowezesha kuwapatia watumishi wa umma nyumba za
kuishi.picha na Freddy Maro.
Comments