Kocha Kim Poulsen akiwaongoza wachezaji wake baada ya kushuka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo.
Taifa Stars imewasili Maputo jana
saa 5 asubuhi kwa saa hapa tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji (The
Mambas) na kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo na Balozi
waTanzania nchini Msumbiji, Balozi Nyandugu.
Stars yenye kikosi cha wachezaji
20 chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen imefikia Hotel 2010 LDA iliyoko
karibu na Uwanja wa Taifa Zimpeto ambapo mechi hiyo itachezwa Jumapili
kuanzia saa 9 kamili kwa saa za hapa ambapoTanzania itakuwa saa 10
kamili.
Kwa mujibu wa programu ya Kocha
Kim, timu itafanya mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya
Jumapili ambayo itachezeshwa na waamuzi kutokaMadagascar. Mpaka timu
inawasili hapa hakuna mchezaji yeyote mwenye matatizo ambayo yanaweza
kusababisha asicheze mechi ya Jumapili.
Boniface Wambura, Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Kwa hisani ya dewjiblog.com
Comments