Katika Tuzo za BET HIPHOP AWARDS zilizofanyika hivi karibuni wimbo wa ''look at me now'' wa Chris Brown ulionekana kuwa gumzo baada ya kuchukua tuzo kadhaa. Wimbo huo ulichukua tuzo ya kuwa na video kali zaidi. Na pia ulikuwa wimbo bora wa kushirikishwa( best collable). Na pia ulichukua tuzo ya kuwa wimbo wenye 'verse' kali zaidi. Bila kusahau ulikuwa wimbo bora uliochaguliwa na watazamaji.
HII YOTE INADHIBITISHA KAMA CHRIS BROWN NI MKALI?
Track ya 'look at me now' inapatikana katika albamu ya Chris Brown ya ''FAME''ambayo aliitoa mwaka huu mwezi februari. Wimbo huu uliandikwa na Chris Brown mwenyewe pamoja na Buster Rhymes,Lil wayne na jamaa wengine wawili ambao ni Diplo,Jean Baptiste,Ryan pamoja na Afrojack. Ingawa Diplo na Afrojack ndio washkaji waliotengeneza wimbo huu wakishirikiana na mkali mwingine aitwaye Free School.
Hii ngoma imefika mpaka kushika namba 6 katika chati maarufu na zinazoheshimika za Billboard Hot 100.
Video yake imetengenezwa na mtu anaitwa Colin Tilley.
Chris Brown kwa sasa anaonekana kuwa juu hususani baada ya kutoa albamu yake ya FAME ambayo inajumuisha nyimbo kadhaa kali kama vile beautiful people,Deuces,she ain't you,na nyingine kali.Inatoka kwa mdau.
Comments