Mwigizaji ‘five star’ kutoka tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper
Masawe, amenyang’anywa ‘mkoko’ (gari) wa kifahari aliokuwa akitanua nao
katika mitaa ya mbalimbali ya jiji la Bongo.Habari zenye ukweli 100%
zinasomeka kuwa Wolper anayejulikana kama Amber Rose wa Bongo
amenyang’anywa mkoko huo aina ya BMW X6 wenye thamani ya ‘ngawira’ za
kibongo ML 170, sambamba na kupigwa ‘stop’ kukaribiana na mshefa
aliyekuwa amemnunulia ndinga hiyo.Kwa mujibu wa chanzo, hatua ya mshefa
huyo kuamua kuchukua ndinga yake ni baada ya kugundua kuwa Wolper
anatoka kimapenzi na ‘sharobaro’ mmoja anayemiliki duka maarufu la
viwalo pande za Kinondoni.Aidha chanzo hicho, kimeieleza kuwa hivi
sasa mwanadada huyo ameamua kutembelea ndinga aina ya Noah aliyokuwa
anaitumia hapo awali sambamba na kutoka kwa kuvizia kukwepa watu wake
wa karibu washitukie mchongo.
Katika kuhakikisha kuwa ukweli... Wolper aligeuka mbongo na kudai kuwa hakuna jambo kama hilo isipokuwa kilichotokea ni kuwa gari limepata matatizo na ameamua kulipeleka ‘garage’.Alipotakiwa kueleza kuwa imekuwaje gari mpya kama ile aipeleke garage tena kwa siku tatu Wolper alisema hivi: “Bwana eeh wee jua liko ‘garage’ hayo maswali mengine mimi sitaki kuayasikia na kama una taka ugomvi endelea kuniuliza” alisema na kuondoka haraka eneo alilokuwa amekaa

Comments