Habari tulizozipata asubuhi hii ni kwamba mwanamuziki wa kizazi kipya
anayekwenda kwa jina la Heri Sameer, maarufu zaidi kwa jina la Mr Blue
amepata mtoto wa kiume baada ya mchumba wake aliyewahi kumtambulisha
kwa jina la Wahida kujifungua jana jijini Dar es salaam.Jina la mtoto
huyo ni Sameer ambalo ni jina la Baba mzazi wa Mr Blue.Blog hii kwa
niaba ya wadau wote wa sanaa inampongeza Blue na kumsisitiza kuwa
makini katika malezi ya kijana wake huyu.
One love!
One love!
Comments