David Beckham ameelezea dhamira
yake ya kutaka kuiongoza timu ya Uingereza itakayoshiriki katika
michuano ya soka katika mashindano ya Olimpiki mwaka huu wa 2012.
Beckham alitia saini mkataba mpya na timu ya
Marekani ya LA Galaxy mapema wiki hii, na kati ya makubaliano
aliyoyafanya ni klabu kumruhusu kushiriki katika mashindano ya London.
"Ningelipenda
sana kuwa nahodha", mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alielezea.
"Nimewahi kuiongoza nchi yangu, na ninaelewa hili ni jambo muhimu sana
katika kuiongoza timu katika Olimpiki."
"Nimezungumza na Stuart Pearce (kocha), lakini bado sijachaguliwa."
Beckham alikuwa ni kati ya watu waliokuwemo
katika kundi la kuongoza kampeni za London za kuandaa mashindano
waliofika Singapore mwaka 2005.
Yeye ni kati ya wachezaji 184 ambao wameandikiwa
barua na chama cha soka cha FA nchini England kuthibitisha kwamba
wataweza kuichezea timu ya Olimpiki.
"Ningelipenda kuwa kati ya wale watakaoshiriki
katika timu ya GB", alielezea, huku akimshukuru Tim Leiweke, rais wa LA
Galaxy, wamiliki AEG, na kocha wa Galaxy Bruce Arena, kwa kumruhusu
kuondoka MLS kwa muda.Source BBC.
Comments