Skip to main content

Udhaifu Wa JK; Tafsiri Yangu






“ OUR President is important; but, he is not Tanzania. All of our people organaized together are Tanzania”- (Julius Nyerere, Julai  29, 1985)

Ndugu zangu,
Watanzania wengi hatuna mazoea ya kusoma, hata makala za magazetini ukiachilia mbali vitabu vya taarifa na hadithi. Ndio, tu wavivu wa kusoma.

Kigong’onda ni aina ya ndege.  Ndege huyu  ana mdomo mrefu na anapenda sana kugongagonga mti kwa mdomo wake. Ndivyo anavyojipatia ridhiki yake. 

Lakini, kwa hulka yake ya kugong’onda kila kilicho mbele yake, basi, hata ukimwekea mti wa chuma porini, kigong’onda atahangaika nao mpaka damu zimtoke mdomoni. Ni hulka yake.  Kiongozi hapaswi kuwa kama kigong’onda.

Kuna hoja mezani juu ya udhaifu wa JK, imetokea Bungeni.  Yumkini, kama mwanadamu, JK ana mapungufu na udhaifu wake, nani asiye na mapungufu na udhaifu? Lakini, tukimzungumzia JK kama taasisi ya ’ Urais’, namwona Rais anayejipambanua na waliomtangulia. Ni  kwa kujitahidi kufanya yale yalo nafuu na yenye manufaa kwa nchi yetu  kwenye mfumo dhaifu uliopo.  

 Wanadamu tunapaswa kuhukumu dhamira ya mtu na si matokeo. Bado namwona JK kama kiongozi mwenye dhamira njema kwa nchi yetu. Nauona ujasiri ndani ya JK. Ni ujasiri wa kufanya yale ambayo, hata ndani ya chama chake hayakuwezekana kufanywa na Mwenyekiti wa chama huko nyuma. Na bila shaka, kuna wahafidhina ndani ya chama chake wanaomwona JK kuwa ni dhaifu kwa mantiki hiyo. Kuna wanaoamini, ndani ya CCM, kuwa Rais wa chama tawala anayekaa na kuongea na wapinzani Ikulu ni Rais dhaifu!

Na hata haya tunayoyashuhudia sasa, yumkini ni matokeo ya dhamira njema ya JK. Naamini, kwa tunavyoenenda sasa, Tanzania atakayoiacha  JK haiwezi tena kurudi kuwa kama ilivyokuwa kwa Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. JK amepanua uhuru wa Watanzania kuchangia fikra zao bila hofu. Siku zote, hofu haijengi nchi.

Maana, tumefika hapa kutokana na mfumo dhaifu unaozaa Serikali dhaifu, unaozaa Bunge dhaifu na unaopelekea pia kuzaa vyama dhaifu vya siasa ikiwamo chama tawala. Na chimbuko lake ni Katiba ya Nchi iliyo DHAIFU. Ndio, tatizo la nchi yetu ni tatizo la kimfumo.

Ni tatizo lililoasisiwa tangu Awamu ya kwanza ya Urais.  Angalia, Katiba yetu inampa nguvu nyingi sana Rais. Tuna bahati tu hajatokea Rais anayeamua kuzitumia ipasavyo nguvu hizo.

Nimeona katuni ya ndugu yangu Masoud Kipanya kwenye gazeti la Mwananchi la jana, Juni 23, 2012.  Kipanya alionyesha foleni ndefu ya wapiga kura Watanzania walio tayari kumpigia kura Rais Dikteta.   

Niliogopeshwa na michango ya  maoni ya Watanzania juu ya katuni ile. Wengi walionekana kuikubali hali hiyo. Kuwa kwao kwa hali ilivyo sasa ni heri kutawaliwa na dikteta kuliko Rais dhaifu!

Inasikitisha na inaogopesha kuona kuwa tumefika hapa. Naamini mimi na wengine wengi tuliokulia enzi za chama kimoja  na Rais mmoja ambaye ni kila kitu, tusingependa kurudi huko tulikotoka. Nikayasoma jukwaa moja maoni ya Mtanzania Ludovic Mwijage aliyejaribu kuonyesha ubaya wa udikteta. Hapo chini nimeweka kitabu cha Mwijage kilicho kwenye maktaba yangu. Kwa mimi niliyesoma kitabu chake, ningeshangaa kama Mwijage angeunga mkono hoja ya kumwona JK dhaifu na kutamani Rais Dikteta.

Ukweli, sisi wa ’ Kizazi Cha Azimio’ tuliwaona wazazi wetu wakiishi katika hali ya hofu na mashaka. Waliishia kunong’ona tu pale walipotaka kuishutumu Serikali na Rais aliye madarakani.

Mjumbe wa nyumba kumi alikuwa ni mtu aliyeogopewa sana.  Huyu  alikuwa ni wakala wa Chama tawala na Serikali. Moja ya majukumu yake ilikuwa ni kuwatambua, katika nyumba zake kumi, wale wote waliokuwa na mitazamo tofauti na ya Serikali na Mkuu wa Nchi. Ni wale walioitwa ’ Wapinga Maendeleo!’. Kuna waliosekwa rumande, kuna waliofungwa magerezani.

Enzi zile viongozi watu wazima walisimama majukwaani na kusema; ” We have a One Party Democracy!” Katika dunia hii hakuna ‘ One Party Democracy’ bali ‘ One Party Dictatorship’. Hata kwenye nyumba mwanamme ukishaoa huwezi tena kutamka juu ya ‘ One Man Family!’- Na watoto wakiingia kwenye familia , nao pia wanatakiwa wawe na sauti.

Afrika Rais anategemea sana wasaidizi wake katika kuifanya kazi yake. Hivyo, mfumo dhaifu huzaa wasaidizi dhaifu pia. Mfano, pale Bungeni hakukuwa na haja yoyote ya mbunge kutolewa nje kwa kutamka ‘ JK ni Dhaifu’.   

Badala yake, ilikuwa fursa kwa wasaidizi wa JK kujenga hoja za kubomoa hoja za mbunge huyo.
Kumtoa Mbunge nje kumemsaidia zaidi kuwasilisha ujumbe wake na hata ukaaminiwa na wengi. Maana, swali la hata wasiofutilia vipindi vya Bunge ni ‘ Kwani huyo Mnyika amesema nini?” Ni yale yale ya Zitto Kabwe kutolewa Bungeni kwa hoja ya Buzwagi. Nakumbuka kumsikia Mzee Malecela akisimama Bungeni na kutamka, kuwa dawa ya kidole chenye kansa ni kukikata!

Malecela na wengine katika CCM walisaidia, kwa kasi ya ajabu, kumtangaza na kumpa umaarufu Zitto Kabwe. Maana, wengi mitaani walitaka kukiona kidole hicho chenye kansa kinachokisumbua chama tawala na kikongwe hapa nchini, CCM.  

 Na mpaka hii leo, CCM wanarudia makosa yale yale ya jana. Na kwanini wanarudia? Ni kwa baadhi ya watendaji, kuingiwa hofu na wimbi hili la mabadiliko, hivyo kutojiamini na hata kufanya yale wanayodhani yatamfurahisha aliyewateua, kumbe, wanamharibia, na wanazidi kukipaka matope chapa chao.
Naam, tunaweza kuondokana na mfumo dhaifu kupitia Katiba mpya ijayo. Inawezekana.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...