Mjini Dortmund, Ujerumani jumamosi 30 Juni 2012
Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU yenye makao
yake kule Ujerumani,wanategemewa kukwea jukwaa la Afro-Ruhr
Festival, siku ya jumamosi 30 Juni 2012 mjini Dortmund,Ujerumani.
Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya inayoongozwa
na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja wa
FFU,itapeleka mzimu wake wote wa dansi katika onyesho hilo kubwa
la aina yake,washabiki wa muziki katika onyesho hilo wanakumbana
"Jino kwa Jino" na makombora ya muziki wa Ngoma Africa band
aka FFU, bendi hiyo kwa sasa inatamba nyimbo zake za "Supu ya Mawe"
,"Uhuru wa Habari" na "Bongo Tambarare" ambazo ipo katika CD ya
"BONGO TAMBARARE" pia zinasikika katika kambi yao FFU
Comments