Na Mwandishi wetu 24th June 2012
- Kwa mwaka kila mjumbe kuvuna zaidi ya milioni 300/-
– Wasio wajumbe yaani watumishi kutumia bilioni 4.3/-
– Sh bilioni 2.0 kulipia nyumba wafanyakazi wa Sekretariati
Serikali imefanya kufuru ya
kutenga Sh. bilioni 40/- kwa ajili ya wajumbe 34 wa Tume ya Kuratibu
Maoni ya Katiba. Kwa mujibu wa kasma ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba
iliyoko kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13.
Iliyopewa jina la Vote Number 8
(Fungu namba 8), wajumbe 34 wa tume hiyo wametengewa posho ya Sh.
bilioni 10 watakayolipwa kwa kipindi cha mwaka mmoja jambo ambalo baadhi
ya wabunge wamesema hawaridhiki na kuhoji serikali inatafuta kitu gani
kwa tume hiyo.
Wajumbe wa kawaida wa tume hiyo
kwa mujibu wa mchanganuo wa bajeti, watalipwa posho ya Sh. karibu
450,000 kwa siku lakini Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Tume fungu
lao ni kubwa zaidi ambalo limeongezewa viburudisho na takrima.
Kwa mujibu wa taarifa za
uchambuzi wa posho hizo, kila mjumbe kuanzia mwaka wa fedha wa Julai
2012 hadi Julai 2013, atakuwa amejikusanyia zaidi ya Sh milioni 294
jambo ambalo baadhi ya wabunge waliohojiwa na NIPASHE Jumapili walisema
ni maajabu ya Firauni.
Pamoja na kuhakikishiwa kuwa na
ukwasi mkubwa, pia wametengewa Sh. milioni 10 kwa ajili ya matibabu kwa
wale ambao wameelezwa kuwa hawapo kwenye utaratibu wa kugharamiwa tiba
na serikali.
Dau kubwa ambalo lipo kwenye
bajeti hiyo kwa mujibu wa wabunge hao ambao wameomba majina yao
yasitajwe, ni kutengwa Sh. milioni 250 zinazodaiwa zitatumika kwa ajili
ya usafi na ulinzi wa ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Comments