Katika
mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza
kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni
vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa
ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya
kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri
kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama
inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.
MAPATO |
SHILINGI MILIONI
| ||
A | Mapato ya ndani |
11,889,078
| |
i)mapato ya kodi (TRA) |
10,232,539
| ||
ii)Mapato yasiyo ya kodi |
1,163,533
| ||
B | Mapato ya Halmashauri |
493,006
|
Zitto akiwasili Bungeni kwa ajili ya kwenda kuwasilisha bajeti ya upinzani. |
Mapato
haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya
kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa
Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu.
Tunaomba
radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha
kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.
Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri wa Fedha na Uchumi Kivuli
19.06.2012
Comments