Mtandao mmoja wa kijamii umeandika kuwa Mwanamke mmoja huko Mississippi Marekani ameishtaki kampuni ya Facebook kwa kuchunguza mawasiliano yake aliyokuwa anayafanya kupitia mtandao huo wa Facebook. Mwanamke huyo anadai kuwa Facebook imekuwa inachunguza mawasiliano yake wakati anapokuwa online na hata hasipokuwa online. Lakini Facebook yenyewe imekataa kuhusika na vitendo hivyo. Hii si mara ya kwanza kwa Facebook kulaumiwa kufanya hivyo.
Hivi karibuni mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks alidai kuwa mtandao wa Facebook sio mtandao salama sana kwa mawasiliano kwa sababu unatumika na watu wa usalama katika kuchunguza mawasiliano ambayo watu wanafanya kila wakati kupitia mtandao huo. Facebook ni mtandao ulioanzishwa na aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Havard Mark Zuckerberg. Na kwa sasa ni mtandao ambao una watumiaji wanaofikia kiasi cha zaidi ya milioni 500 duniani kote.
Facebook sio mtandao wa kwanza kushtakiwa kwa kuingilia mawasiliano ya watumiaji wake. Na hali hii imeonekana kuendelea kuwa kubwa baada ya hivi karibuni Mark Zuckerberg kuanzisha mfumo mwingine unaoitwa Timeline and Ticker features.
Comments