WAKATI
mwenyekiti wa Simba, Ismail aden Rage akijigamba kulijumuisha jina la
mchezaji Kelvin Yondani katika usajili, habari ambazo Mwananchi
imezipata, ni kwamba klabu hiyo imeamua kuachana na mchezaji huyo.
Simba
ilikuwa ikihaha kumnusuru beki huyo ambaye amekwishajichomoza Yanga na
hata kuanza mazoezi wakitaka kumrejeshea fedha zake apeleke Yanga na
arudi kundini.
Hatua
hiyo ilifikiwa baada ya Yondan kuanza mazoezi Yanga, na viongozi na
wadau wakubwa wa Simba walikuwa katika hekaheka za kumrudisha kundini.
Awali
Habari ambazo Mwananchi ilizipata zilidai kuwa mdau mmoja wa Simba
alikutana na wadau na viongozi wa Simba pamoja na Yondani mwenyewe
wakimshawisi wampatie fedha, kiasi alichochukua ili azirejeshe Yanga.
Chanzo
cha habari kinasema kuwa wadau na wapenzi wa Simba hawakuridhishwa na
hatua ya beki huyo kwenda Yanga na kwamba anahitajika kwa kiasi kikubwa
Simba.
Baada
ya Yondani kuonyesha kuanza mapenzi mapya na Yanga, watu wa karibu wa
Simba wamepitisha azimia la kuachana na beki huyo huku wakiamini kuwa
wachezaji waliopo wanaweza kuvaa viatu vyake.
"Tumeamua
kuachana na Yondani baada ya kumuona Lino Musonda, anacheza vizuri beki
wa kati na tunaamini atatusaidia," kilipasha chanzo hicho.
Kiliendelea
kudai chanzo hicho kuwa, wasiwasi mkubwa ulikuwa beki wa kati lakini
baada ya kupatikana Musonda, kwa pamoja waliridhia beki huyo aende
akacheze soka Yanga.
Wakati
hayo yakijiri jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage alikaririwa na
Mwananchi Jumapili akikazia kusema Yondani amekwenda Yanga kutia
mashamsham ya mazoezi lakini bado ni mchezaji wao halali.
"Yanga
wanajifurahisha wenyewe na kelele zao kamwe hazinitishi...mimi nasema
mbivu na mbichi vitajulikana Juni 30 tutakapoweka hadharani kikosi chetu
kitakashiriki Ligi Kuu msimu ujao," alisema Rage.
Katika
hatua nyingine, kocha wa Simba, Milovan Cirkovic aliyewasili jijini Dar
es Salaam juzi usiku akitokea Serbia alikokuwa kwa mapuziko, anatarajia
kuanza mikakati yake leo ya kuinoa Simba kwa Michuano ya Kagame
iliyopangwa kuanza kutimua vumbi Julai 14 mwaka huu.
Kocha
huyo pia ataitumia nafasi hiyo kuangalia uwezo wa wachezaji wapya wa
kikosi hicho ambao walisajiliwa na hivi karibuni bila ya yeye kuwepo
licha ya uongozi wa kilabu hiyo kudai kuwa ulikuwa umepata baraka zake
zote.
Kikosi
cha mabingwa hao wa Ligi Kuu ambacho kilikuwa katika mikoa ya Kanda ya
Ziwa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Michuano ya Kagame.
Ofisa
Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa timu hiyo haina muda wa
kupoteza kwa sasa na leo jioni itaendelea na mzoezi yake kwenye Viwanja
vya Klabu ya Sigara, TCC, Chang’ombe, Dar es Salaam.
Comments