Kupitia blog moja ya kijamii mwana blog amemlenga gwiji wa muziki wa Marekani na kafunguka kuwa , Mc Hammer sasa ameingia kwenye mambo ya teknolojia baada ya kutangaza kuanzisha search engine iitwayo 'WireDoo'. Mc Hammer alitangaza kuanzishwa kwa search engine hiyo katika mkutano mkubwa unaoitwa WEB 2.0 huko San Fransisco Marekani. Kwa mujibu wa Mc Hammer amesema WireDoo itakuwa inatumika kutafuta topiki au vitu mbalimbali mfano magari na vitu vingine tofauti.
Mc Hammer ambaye alikuwa ni mkali wa Hiphop aliyefunika mbaya miaka hiyo? kwa sasa anajishughulisha na mambo ya teknolojia. Na ameshaudhuri kwenye vyuo mbalimbali kutoa mihadhara (presentations) ikiwemo Oxford University cha England na Harvard cha Marekani.
Kwa sasa hivi Google ndio kila kitu,pale unapozungumzia social engine kali. Je WireDoo inaweza ikaipiga bao Google????
Comments