JANA katika ukumbi wa Makumbusho, katikati ya Jiji la Dar es Salaam, mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), kulikuwa kuna onyesho la Miss Dar Inter College.
BIN ZUBEIRY alikuwepo na kamera yake katika onyesho hilo, ambalo Jaji Mkuu alikuwa Miss Tanzania wa 2006, Wema Sepetu huku mpenzi wake wa zamani, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’ akitumbuiza.
Shoo ilichelewa kuanza kidogo hadi mida ya saa sita usiku- na baada ya warembo kucheza shoo ya ufunguzi, kupita na vazi la ubunifu na la jioni, kabla ya tano bora kutangazwa, ilikuwa zamu ya Platinum wa bongo kupanda katika stage.
Taa zilizimwa na kijana akaibuka na madansa wake jukwaani. Lakini wakati tu MC anasema anamuita Diamond, mapigo ya moyo ya Jaji Mkuu, yalionekana kubadilika na kwenda kasi.
Kwa muda wote, Majaji wenzake wawili walikuwa wanawasiliana naye, lakini ilionekana ghafla kama yeye amekata mawasiliano nao.
Kulikuwa kuna dalili za kutosha kusema; Wema alichanganyikiwa. Dida wa Times FC aliyekuwa jaji pia, alijitahidi kadiri ya uwezo wake kumfanya Wema awe katika hali ya kawaida, lakini alishindwa.
Wema alishindwa kujimudu. Kulikuwa kuna dalili zsa kutosha kusema Wema anampenda sana Diamond. Alikuwa anamfuatilia kwa kila hatua. Alikuwa anaingiwa na kuguswa na nyimbo za Wema Wangu, Mawazo na Nimpende Nani alizokuwa anaimba Diamond pale jukwaani.
Diamond naye sasa; ilionekana dhahiri kila anachokifanya jukwaani ni kwa ajili ya Wema. Na alikuwa anaomba sapoti ya mashabiki ili kujiridhisha kama yuko sahihi.
Kwa sisi waswahili huwezi kusita kusema Diamond alikuwa anampiga ‘vikoleo’ aka vijembe Wema. Lakini pamoja na yote, Diamond alionekana kuwasilisha hisia zake kwamba hakuwa tayari kuachana na Wema.
Ni kama kuna kitu kilimsukuma kujitoa katika mahusiano. Ni nini hicho? Kitendawili kigumu.
Ikumbukwe wawili hawa walifikia hadi kuvalishana pete ya uchumba lakini ndani ya miezi michache tu, penzi likavunjika.
Ila, ndani ya mioyo yao kuna siri nzito sana na kinachoonekana anakosekana jasiri tu kati yao wa kumuanza mwenzake kuhusu mada ya kurejesha uhusiano wao.
Wanaonekana wanapendana bado, na haitakuwa ajabu siku moja wakirudiana. BIN ZUBEIRY mwenye uzoefu wa kutosha juu ya masuala ya mahusiano, raha na maumivu ya mapenzi, anawoambea wawili hao, siku moja wawe mwili mmoja tena. Mungu wabariki na wafungue, waondolee uzito Wema na Diamond. Siku moja, waitane wife n husband. Inshaallah. True love never die.
Comments