Na Himid Choko , BLW
Spika wa Baraza la Wawakilishi
la Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho amesema wajumbe wa Baraza hilo
Wamekabidhiwa majukumu makubwa na wananchi hivyo ni lazima wawe na
uelewa mpana juu ya mambo mbali mbali yanayohusu mustakbali wa maisha ya
wananchi.
Mhe. Kificho ametaja baadhi ya
majukumu hayo kua ni pamoja na utungaji wa sheria, kuidhinisha bajeti ya
Serikali ya kila mwaka, kuihoji na kuidhinisha mipango ya maendeleo ya
Serikali ambayo italenga matakwa ya wananchi kwa ajili ya maendeleo yao.
Mhe. Kificho amesema hayo leo
wakati akifungua semina ya siku moja ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
iliyojadili Ripoti ya Wataalamu kuhusiana uwezo wa wajumbe katika
masuala ya utungaji wa sheria na “Data Base” za Wadau wa Kamati za
Kudumu za Baraza la Wawakilishi katika hoteli Ya Coconut Tree Village
Marumbi, wilaya ya Kati , Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema kutokana na majukumu hayo mazito ni vyema kwa Wajumbe wa Baraza hilo kuwa na uelewa mpana katika mambo wanayo yasimamia.
Comments