Annan aelezea matumaini juu ya mkutano wa Syria
Juhudi za kidiplomasia zinaendelea
kujaribu kuuokoa mpango wa amani wa Syria siku moja kabla ya mkutano
mwingine wa kimataifa ambao unaandaliwa mjini Geneva kutafuta suluhu ya
mgogoro uliodumu kwa miezi 16 nchini Syria.
Kikwazo kikubwa kwa mkutano huo
ni msimamo wa Urusi kusisitiza mabadiliko yafanywe katika mpango wa Kofi
Annan, ambao unataka kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini
Syria, ambayo itashirikisha wajumbe kutoka upande wa serikali na ule wa
waasi.
Hata hivyo mpango huo uneeleza
kuwa wajumbe watakaokubaliwa kutoka upande wa serikali, ni wale ambao
kushiriki kwao hakuwezi kukwamisha mchakato wa kuleta utengamano na
maridhiano.
Wanadiplomasia kutoka nchi za
magharibi, wamemueleza Kofi Annan kuwa mkutano huo wa Jumamosi mjini
Geneva hautakuwa na maana yoyote, hadi pale maafikiano yatakapofikiwa
baina ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton na
mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov ambao watakutana leo jioni mjini
Petersburg, Urusi.
Urusi yataka marekebisho
Urusi, kupitia waziri wake wa
mambo ya nchi za nje, inasema mkutano wa Geneva unapaswa kuunga mkono
mazungumzo baina ya wasyria wenyewe, bila kuamua juu ya mada ya
mazungumzo hayo.
Comments