Kamanda
wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na
kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka
anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya
Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda
Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka
kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema
huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa
kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua
maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa
ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda
Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa
ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni
tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote
watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na
sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo
Waandishi wa habari waimsikilza kamanda Suleiman Kova katika kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es salaam leo mchana.
Chanzo: http://www.fullshangweblog.com
Comments