MSANII mahiri katika tasnia ya filamu nchini Jimmy Mponda 'Jimmy
Master''amefunguka' na kusema sasa ajira nyingi zitazidi kuongezeka kupitia filamu kwa
siku za usoni
Akizungumza Dar es Salaam Jimmy Master alisema kuwa hali ya kuongezeka huko inakuja baada ya yeye mwenyewe kupitia kampuni yake ya Jimpowood kutoa mafunzo kwa wasanii chipukizi.
"Kupitia uzoefu wangu katika tasnia ya filamu kwa sasa natoa mafunzo ya sanaa,"alisema 'Jimmy Master'
Alisema tayari amesha toa ajira kwa wasanii 60 , ambao wamepita katika
mafunzo yake yanayofanyika kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa katika nyakati za jioni kupitia ofisi zake zilizopo DDC Magomeni.
Jimmy Master alisema kuwa , katika ujio wake wa filamu ya sasa iitwayo
'Doble -J' ameweza kuwashirikisha wasanii waliopata mafunzo anayoyatoa.
Msanii huyo alisema katika mafunzo yake hayo utoza malipo kwa miezi mitatu kwa garama ya shilingi sh 30,000 .
Aidha Jimmy alitaja baadhi ya wanafunzi kati ya hao 60 waliopata ajira baada ya kupata mafunzo hayo kuwa ni Sebastian Marco , Veronica Vyankero ,Angele Maigi , Kharid Ramadhan.
Pia aliwataja wengine kuwa ni Amor Juma Quee Karebi , Hammed Juma
na kusema wasanii hao wameweza kuuvaa uhusika katika filamu hiyo ya 'Doble J' ambayo tayari imetoka matoleo matatu na kutua katika soko la filamu Bongo.
Comments