Leo asubuhi Mhe. Dk. Jakaya M. Kikwete , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliwakaribisha ikulu viongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF).
Viongozi wa TBF waliokuwepo ni Musa Mziya Rais wa TBF, Phares Magesa Makamu Rais wa TBF, Michael Maluwe Katibu Msaidizi wa TBF na Marry Mmbaga Mhazini wa TBF, pia alikuwepo ndugu Matoke Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo toka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Vijana na Michezo.
Makamu wa Rais wa TBF ndugu Phares Magesa kwa niaba ya TBF na kwa niaba ya Kocha Greg Brittenham alitoa maelezo mafupi na kumkabibidhi Rais Kikwete Jersey rasmi ya timu ya New York Knicks yenye jina la KIKWETE ambayo ilitolewa na Kocha Greg ambaye alikuwa nchini kuendesha mafunzo ya kikapu kwa vijana nchini ya miaka 17 yaliyofanyika Arusha 9-10 Juni, 2012 na kushirikisha vijana 100 kati yao wa kike 30 na wa kiume 70.
Pia ndugu Magesa alimkabidhi Mhe. Rais Jacket maalumu la viongozi wa michezo kutoka chuo Kikuu cha Wake Forest ambako Kocha Greg kwa sasa ni Mkurugenzi wa michezo, kabla ya kuijunga na chuo hiki Kocha Greg alikuwa ni kocha Msaidizi wa New York Knicks kwa miaka 20 na ni moja ya makocha bora sana na wa daraja wa juu kabisa duniani wa kikapu katika Strenth and Conditioning.
Pia Rais wa TBF Mziya amkabidhi Mhe. Rais Kikwete Mpira wa kikapu toka kwa wadau wa TBF Kampuni ya Coca Cola kupitia kinywaji cha SPRITE. Mhe.
Rais alishukuru TBF, Kocha Greg , Timu ya New York Knicks, Chuo Kikuu Cha Wake Forest na Coca Cola kwa vifaa hivyo vya michezo na akaomba tuimarishe mahusiano nao ili kuinua mchezo wa kikapu nchini.
Kutoka Full Shangwe. www.fullshangwe.com
Comments