JUMUIYA ya Madaktari imetangaza rasmi kuanza kwa mgomo usio na
kikomo kuanzia kesho, huku ikidai Serikali imekataa kutekeleza madai
yao yote yaliyowasilishwa katika kamati ya majadiliano iliyoundwa na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Wakati madaktari hao wakitangaza kurejea
rasmi katika mgomo huo uliositishwa miezi mitatu iliyopita, Pinda
aliliambia Bunge jana wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo, kuwa
mgomo huo ni batili na haukubaliki.
Saa chache baada ya Pinda kutoa onyo hilo lililorushwa moja kwa moja
na vituo vya televisheni na redio kutoka Dodoma, madaktari hao wakiwa
jijini Dares Salaam walitangaza mgomo huo wenye lengo la kushinikiza
Serikali kutekeleza madai yao.
Mgomo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari na Dk Stephen
Ulimboka, muda mfupi baada ya kukamilika kwa mkutano wa ndani wa
madaktari, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Utamaduni
la Watu wa Urusi.
Dk Ulimboka alisema mgomo huo usio na kikomo utawahusu madaktari wa
kada zote nchini, na unatarajiwa kuanza kesho, baada ya wiki mbili
walizotoa kwa Serikali kumalizika bila ya makubaliano yoyote.
“Madaktari kwa ujumla wao wamekubaliana kuwa watarejea katika mgomo
usio na kikomo, hii ni kutokana na kugundua kuwa hakuna dhamira ya
dhati ya Serikali, kumaliza mgogoro kati yetu na Serikali, uliodumu kwa
muda mrefu sasa,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza,
Read more: BongoCelebrity
Comments